2 Chronicles 16:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa ufalme wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu, akaugua sana. Lakini hata wakati huo, Asa hakumgeukia Mwenyezi-Mungu amsaidie, bali alijitafutia msaada kutoka kwa waganga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alishikwa na ugonjwa kwa miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu bali kwa matabibu tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa ufalme wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu, akaugua sana. Lakini hata wakati huo, Asa hakumgeukia Mwenyezi-Mungu amsaidie, bali alijitafutia msaada kutoka kwa waganga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa BWANA bali kwa matabibu tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa bwana bali kwa matabibu tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada kwa waganga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa ufalme wake, Asa alishikwa na ugonjwa wa miguu, akaugua sana. Lakini hata wakati huo, Asa hakumgeukia Mwenyezi-Mungu amsaidie, bali alijitafutia msaada kutoka kwa waganga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa 39 wa ufalme wake Asa akaugua miguu, huu ugonjwa wake ukazidi sana; namo katika huu ugonjwa wake hakumtafuta Bwana, ila waganga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali waganga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa makumi tatu na kenda wa utawala wake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu. Ugonjwa ule ukazidi sana kuongezeka. Lakini hata wakati ule, Asa hakumugeukia Yawe amusaidie, lakini alijitafutia musaada kutoka kwa waganga.