2 Chronicles 16:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alizikwa katika kaburi alilokuwa amejichimbia mwenyewe mwambani, katika mji wa Daudi. Walimlaza ndani ya jeneza lililokuwa limejazwa manukato ya kila aina yaliyotayarishwa na mafundi wa kutengeneza marashi, wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amejichongea katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezo na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakamfukizia mafukizo makuu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alizikwa katika kaburi alilokuwa amejichimbia mwenyewe mwambani, katika mji wa Daudi. Walimlaza ndani ya jeneza lililokuwa limejazwa manukato ya kila aina yaliyotayarishwa na mafundi wa kutengeneza marashi, wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amelichonga kwa ajili yake mwenyewe katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezi na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amejichongea mwenyewe katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezi na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alizikwa katika kaburi alilokuwa amejichimbia mwenyewe mwambani, katika mji wa Daudi. Walimlaza ndani ya jeneza lililokuwa limejazwa manukato ya kila aina yaliyotayarishwa na mafundi wa kutengeneza marashi, wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamzika penye makaburi yake, aliyojichimbia mjini mwa Dawidi; wakamlaza katika kilalo walichokijaza uvumba wa namna nyingi na manukato yaliyotengenezwa na mafundi, wakamvukizia mavukizo makubwa sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakamfukizia mafukizo makuu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akazikwa katika kaburi alilokuwa amejichimbia yeye mwenyewe, katika muji wa Daudi. Walimulalisha juu ya kitanda kilichokuwa kimejazwa marasi ya kila aina yaliyotayarishwa na wafundi wa kutengeneza marasi, wakawasha moto mukubwa sana kwa heshima yake.