2 Chronicles 16:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ikulu, akazituma Damasko kwa Ben-hadadi, mfalme wa Aramu na ujumbe akasema,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka hazina ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na kutoka jumba lake la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, aliyekuwa anatawala huko Dameski.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ikulu, akazituma Damasko kwa Ben-hadadi, mfalme wa Aramu na ujumbe akasema,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka katika hazina ya Hekalu la BWANA na kutoka katika jumba lake mwenyewe la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye alikuwa anatawala huko Dameski.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka hazina ya Hekalu la bwana na kutoka jumba lake mwenyewe la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye alikuwa anatawala huko Dameski.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo mfalme Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ikulu, akazituma Damasko kwa Ben-hadadi, mfalme wa Aramu na ujumbe akasema,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Asa alipochukua fedha na dhahabu katika vilimbiko vya Nyumba ya Bwana na vya nyumba ya mfalme, akazituma kwake Benihadadi, mfalme wa Ushami, aliyekaa Damasko, kumwambia:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo mufalme Asa akatwaa feza na zahabu kutoka katika hazina ya nyumba ya Yawe na ya nyumba ya kifalme, akazituma Damasiki kwa Beni-Hadadi, mufalme wa Suria, na ujumbe akasema: