2 Chronicles 16:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na tufanye mkataba wa ushirikiano kati yangu na wewe kama walivyofanya baba yangu na baba yako; tazama nakupa zawadi ya fedha na dhahabu; nenda ukavunje mkataba wa ushirikiano ulioko kati yako na mfalme Baasha wa Israeli ili aache mashambulizi dhidi yangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Na pawe mkataba kati yangu na wewe, kama palivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwangu na kwako na liwe agano kama lilivyokuwa kwa baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea fedha na dhahabu; basi, uvunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na tufanye mkataba wa ushirikiano kati yangu na wewe kama walivyofanya baba yangu na baba yako; tazama nakupa zawadi ya fedha na dhahabu; nenda ukavunje mkataba wa ushirikiano ulioko kati yako na mfalme Baasha wa Israeli ili aache mashambulizi dhidi yangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Pawepo na makubaliano kati yangu na wewe, kama yalivyokuwako kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, ninakupelekea fedha na dhahabu. Basi vunja makubaliano yako na Mfalme Baasha wa Israeli ili aweze kujiondoa huku kwangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Pawepo na mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na pawepo agano la kushirikiana kati yangu na wewe kama lilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako; tazama, nimekutumia fedha na dhahabu; basi, uvunje mkataba wako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aache kunishambulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na tufanye mkataba wa ushirikiano kati yangu na wewe kama walivyofanya baba yangu na baba yako; tazama nakupa zawadi ya fedha na dhahabu; nenda ukavunje mkataba wa ushirikiano ulioko kati yako na mfalme Baasha wa Israeli ili aache mashambulizi dhidi yangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Liko agano, tuliloliagana mimi na wewe, naye baba yangu na baba yako; kwa hiyo ninatuma kwako fedha na dhahabu. Nenda, ulivunje agano, uliloliagana na Basa, mfalme wa Waisiraeli, aondoke kwangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwangu na kwako na liwe agano kama lilivyokuwa kwa baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea fedha na dhahabu; basi, uvunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Tufanye mapatano ya ushirikiano kati yangu na wewe kama vile baba yangu na baba yako walivyofanya. Angalia ninakutumia zawadi ya feza na zahabu, kwenda uvunje mapatano ya ushirikiano unaokuwa kati yako na mufalme Basha wa Israeli kusudi aache mashambulizi juu yangu.”