2 Chronicles 16:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu huuchunga kwa makini ulimwengu wote, ili kuwapa nguvu wale walio waaminifu kwake. Umetenda jambo la kipumbavu, kwa hiyo tangu sasa, utakuwa na vita kila mara.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa macho ya Mwenyezi Mungu yanazunguka dunia yote ili kuwatia nguvu wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu, na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu huuchunga kwa makini ulimwengu wote, ili kuwapa nguvu wale walio waaminifu kwake. Umetenda jambo la kipumbavu, kwa hiyo tangu sasa, utakuwa na vita kila mara.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa macho ya BWANA hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa macho ya bwana hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu huuchunga kwa makini ulimwengu wote, ili kuwapa nguvu wale walio waaminifu kwake. Umetenda jambo la kipumbavu, kwa hiyo tangu sasa, utakuwa na vita kila mara.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani macho ya Bwana huzunguka katika nchi zote, ajitokeze kuwa mwenye nguvu kwao waliomwelekezea mioyo yao yote mizima. Katika jambo hili umefanya upumbavu, kwa hiyo tangu sasa huna budi kupiga vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anachunga kwa uangalifu ulimwengu wote, kwa kuwapa nguvu wale wanaokuwa waaminifu kwake. Umetenda jambo la kipumbafu, kwa hiyo tangu sasa, utakuwa na vita kila mara.”