2 Chronicles 17:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ndiyo orodha yao kulingana na koo za baba zao: Adna alikuwa kamanda wa vikosi vya askari 1,000 wa kabila la Yuda. Chini yake, kulikuwa na askari laki tatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: Jemadari Adna akiwa na wapiganaji elfu mia tatu;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ndiyo orodha yao kulingana na koo za baba zao: Adna alikuwa kamanda wa vikosi vya askari 1,000 wa kabila la Yuda. Chini yake, kulikuwa na askari laki tatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, makamanda wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa elfu mia tatu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ndiyo orodha yao kulingana na koo za baba zao: Adna alikuwa kamanda wa vikosi vya askari 1,000 wa kabila la Yuda. Chini yake, kulikuwa na askari laki tatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakijipanga kwa milango ya baba zao, ikawa hivyo: Wayuda walikuwa na wakuu wa maelfu, mkuu mwenyewe ni Adina, pamoja naye wakawa mafundi wa vita wenye nguvu 300000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo hesabu yao kulingana na ukoo za babu zao: Adina alikuwa jemadari wa vikundi vya waaskari elfu wa kabila la Yuda. Chini yake, kulikuwa waaskari elfu mia tatu.