2 Chronicles 18:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mikaya akasema, “Niliwaona watu wote wa Israeli wametawanyika milimani kama kondoo wasio na mchungaji. Naye Mwenyezi-Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi; waache warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Mwenyezi Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mikaya akasema, “Niliwaona watu wote wa Israeli wametawanyika milimani kama kondoo wasio na mchungaji. Naye Mwenyezi-Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi; waache warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye BWANA akasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye bwana akasema, ‘Watu hawa hawana bwana. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mikaya akasema, “Niliwaona watu wote wa Israeli wametawanyika milimani kama kondoo wasio na mchungaji. Naye Mwenyezi-Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi; waache warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, aliposema: Nimewaona Waisiraeli, nao walikuwa wametawanyika milimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Bwana akasema: Hawa hawana bwana, na warudi na kutengemana kila mtu nyumbani kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Mikaya akasema: “Niliwaona watu wote wa Israeli wakitawanyika juu ya milima kama kondoo wasiokuwa na muchungaji. Naye Yawe akasema: ‘Watu hawa hawana kiongozi; uwaache warudi kila mutu kwake kwa amani.’ ”