2 Chronicles 18:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miaka kadhaa Yehoshafati alikwenda Samaria kumtembelea mfalme Ahabu. Ahabu akamchinjia Yehoshafati kondoo na ng'ombe wengi, kwa heshima yake pamoja na watu waliokuwa pamoja naye, kisha akamshawishi aandamane naye kuushambulia mji wa Ramoth-gileadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya miaka kadhaa akateremka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ng’ombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata baada ya miaka kadha wa kadha akamshukia Ahabu huko Samaria. Ahabu akamchinjia kondoo na ng'ombe tele, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, akamshawishi ili apande pamoja naye waende Ramoth-gileadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miaka kadhaa Yehoshafati alikwenda Samaria kumtembelea mfalme Ahabu. Ahabu akamchinjia Yehoshafati kondoo na ng'ombe wengi, kwa heshima yake pamoja na watu waliokuwa pamoja naye, kisha akamshawishi aandamane naye kuushambulia mji wa Ramoth-gileadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya miaka kadhaa akashuka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ng'ombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya miaka kadhaa akashuka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ng’ombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata baada ya miaka kadhaa akamshukia Ahabu huko Samaria. Ahabu akamchinjia kondoo na ng'ombe tele, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, akamshawishi ili apande pamoja naye waende Ramoth-gileadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya miaka kadhaa Yehoshafati alikwenda Samaria kumtembelea mfalme Ahabu. Ahabu akamchinjia Yehoshafati kondoo na ng'ombe wengi, kwa heshima yake pamoja na watu waliokuwa pamoja naye, kisha akamshawishi aandamane naye kuushambulia mji wa Ramoth-gileadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miaka ilipopita michache, akashuka kwenda Samaria kwake Ahabu; Ahabu akamchinjia yeye na watu wake, aliokuwa naye, mbuzi na kondoo na ng'ombe wengi, akamchochea kupanda Ramoti wa Gileadi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata baada ya miaka kadha wa kadha akamshukia Ahabu huko Samaria. Ahabu akamchinjia kondoo na ng’ombe tele, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, akamshawishi ili apande pamoja naye waende Ramoth-gileadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya miaka fulani Yosafati akakwenda Samaria kumutembelea mufalme Ahabu. Ahabu akamuchinjia Yosafati kondoo na ngombe wengi, kwa heshima yake pamoja na watu waliokuwa pamoja naye, kisha akamushawishi aende pamoja naye kwa kushambulia muji wa Ramoti-Gileadi.