2 Chronicles 18:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo nabii Sedekia mwana wa Kenaana akamkaribia Mikaya, akampiga kofi shavuni na kumwuliza, “Kwa njia gani Roho wa Mwenyezi-Mungu ameniacha na akaja kunena nawe?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Mwenyezi Mungu alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya Bwana ili aseme na wewe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo nabii Sedekia mwana wa Kenaana akamkaribia Mikaya, akampiga kofi shavuni na kumwuliza, “Kwa njia gani Roho wa Mwenyezi-Mungu ameniacha na akaja kunena nawe?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Zedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa BWANA alipita njia gani, alipotoka kwangu ili kusema nawe?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa bwana alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu Roho ya BWANA ili aseme na wewe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo nabii Sedekia mwana wa Kenaana akamkaribia Mikaya, akampiga kofi shavuni na kumwuliza, “Kwa njia gani Roho wa Mwenyezi-Mungu ameniacha na akaja kunena nawe?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sedekia, mwana wa Kenaana, alipomkaribia Mikaya, akampiga makofi na kumwuliza: Roho ya Mungu imeshika njia gani, inipite mimi, ije kusema na wewe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya BWANA ili aseme na wewe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nabii Zedekia mwana wa Kenana akamukaribia Mikaya, akamupiga kofi kwenye shavu na kumwuliza: “Kwa njia gani Roho wa Yawe ameniacha na akakuja kusema nawe?”