2 Chronicles 18:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye makapteni hao walipomwona Yehoshafati, walisema, “Huyu mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo, walimwelekea kumshambulia; lakini Yehoshafati akapiga kelele, na Mwenyezi-Mungu akamwokoa. Mungu akawaondoa wale waliokuwa karibu kumshambulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, naye Mwenyezi Mungu akamsaidia. Mungu akawaondoa kwake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa maakida wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na Bwana akamsaidia; Mungu akawafarakisha kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye makapteni hao walipomwona Yehoshafati, walisema, “Huyu mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo, walimwelekea kumshambulia; lakini Yehoshafati akapiga kelele, na Mwenyezi-Mungu akamwokoa. Mungu akawaondoa wale waliokuwa karibu kumshambulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, naye bwana akamsaidia. Mungu akawaondoa kwake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa makamanda wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na BWANA akamsaidia; Mungu akawaondoa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye makapteni hao walipomwona Yehoshafati, walisema, “Huyu mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo, walimwelekea kumshambulia; lakini Yehoshafati akapiga kelele, na Mwenyezi-Mungu akamwokoa. Mungu akawaondoa wale waliokuwa karibu kumshambulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, wakuu wa magari walipomwona Yosafati wakamwazia yeye kuwa mfalme wa Waisiraeli, wakamzunguka kupigana naye. Ndipo, Yosafati alipopiga yowe, Bwana akamsaidia, yeye Mungu akawaondoa hapo, alipokuwa, na kuwadanganyadanganya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa maakida wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na BWANA akamsaidia; Mungu akawafarakisha kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakubwa wale walipomwona Yosafati, wakasema: “Huyu ndiye mufalme wa Israeli.” Kwa hiyo, wakamwelekea kwa kumushambulia; lakini Yosafati akapiga kelele, na Yawe akamwokoa. Mungu akawaondoa wale waliokuwa karibu kumushambulia.