2 Chronicles 18:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini askari mmoja wa Aramu akauvuta upinde wake kwa kubahatisha, mshale ukamchoma mfalme wa Israeli katika nafasi ya kuungana kwa vazi lake la chuma. Hapo Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Nimejeruhiwa! Geuza gari uniondoe vitani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma. Mfalme akamwambia mwendesha gari lake la vita, “Geuza gari na uniondoe katika mapigano, nimejeruhiwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini askari mmoja wa Aramu akauvuta upinde wake kwa kubahatisha, mshale ukamchoma mfalme wa Israeli katika nafasi ya kuungana kwa vazi lake la chuma. Hapo Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Nimejeruhiwa! Geuza gari uniondoe vitani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma, mfalme akamwambia mwendesha gari lake, “Geuza gari na uniondoe mimi katika mapigano, nimejeruhiwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari, Geuza gari, uniondoe katika vita; kwa kuwa nimejeruhiwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini askari mmoja wa Aramu akauvuta upinde wake kwa kubahatisha, mshale ukamchoma mfalme wa Israeli katika nafasi ya kuungana kwa vazi lake la chuma. Hapo Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Nimejeruhiwa! Geuza gari uniondoe vitani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na mtu, akauvuta upindi wake kwa kubahatisha tu, akampiga mfalme wa Waisiraeli hapo, vyuma vya kisibau chake vilipounganishwa. Ndipo, alipomwambia mwendeshaji wa gari: ligeuze kwa mkono wako, unitoe hapa, wanapopigana, kwani nimeumia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini askari mumoja wa Suria akauvuta upinde wake, kwa kubahatisha, akamupiga mufalme wa Israeli mushale katika nafasi ya maunganio ya nguo yake ya chuma ya kujikinga kifua. Hapo Ahabu akamwambia mwongozi wa gari lake la vita: “Geuza gari uniondoe katika vita nimeumizwa.”