2 Chronicles 18:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nayo mapigano siku hiyo, yakazidi kuwa makali huku mfalme wa Israeli amejiegemeza mwenyewe garini akiwaelekea Washamu mpaka jioni. Halafu mnamo machweo ya jua, alifariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vita vikaendelea mchana kutwa, naye mfalme wa Israeli akajitegemeza ndani ya gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Basi jioni yake akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pigano likazidi siku ile; lakini mfalme wa Israeli akajitegemeza garini juu ya Washami hata jioni; akafa kama wakati wa kuchwa kwa jua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nayo mapigano siku hiyo, yakazidi kuwa makali huku mfalme wa Israeli amejiegemeza mwenyewe garini akiwaelekea Washamu mpaka jioni. Halafu mnamo machweo ya jua, alifariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vita vikaendelea mchana kutwa naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari kuelekea Waaramu. Damu kutoka kwenye jeraha lake ikachuruzika ndani ya gari na jioni yake akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vita vikaendelea mchana kutwa, naye mfalme wa Israeli akajitegemeza ndani ya gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Basi jioni yake akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pigano likazidi siku ile; lakini mfalme wa Israeli akajitegemeza garini juu ya Washami hata jioni; akafa kama wakati wa kuchwa kwa jua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nayo mapigano siku hiyo, yakazidi kuwa makali huku mfalme wa Israeli amejiegemeza mwenyewe garini akiwaelekea Washamu mpaka jioni. Halafu mnamo machweo ya jua, alifariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mapigano yakazidi siku hiyo, kwa sababu hii mfalme wa Waisiraeli alikuwa amejisimamisha garini ng'ambo ya huku kuwaelekea Washami hata jioni, akafa, jua lilipokuchwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pigano likazidi siku ile; lakini mfalme wa Israeli akajitegemeza garini juu ya Washami hata jioni; akafa kama wakati wa kuchwa kwa jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nayo mapigano siku ile, yakazidi kuwa makali wakati mufalme wa Israeli amejiegemeza mwenyewe ndani ya gari akiwaelekea Wasuria mpaka magaribi. Halafu wakati jua liliposhuka, akakufa.