2 Chronicles 18:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Yupo bado mmoja, Mikaya mwana wa Imla. Yeye twaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu. Lakini namchukia kwa sababu yeye kamwe hatabiri jambo jema juu yangu, ila mabaya tu.” Yehoshafati akamwambia, “Si vizuri mfalme kusema hivyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia kwake twaweza kuuliza ushauri wa Mwenyezi Mungu, lakini namchukia kwa sababu hatabiri jambo lolote jema kunihusu, ila hunitabiria mabaya kila mara. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza Bwana kwa yeye; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Yupo bado mmoja, Mikaya mwana wa Imla. Yeye twaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu. Lakini namchukia kwa sababu yeye kamwe hatabiri jambo jema juu yangu, ila mabaya tu.” Yehoshafati akamwambia, “Si vizuri mfalme kusema hivyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumwuliza shauri la BWANA, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lo lote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia yeye twaweza kumuuliza shauri la bwana, lakini namchukia kwa sababu huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu mimi, lakini kila mara hunitabiria mabaya tu. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza ya BWANA; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Yupo bado mmoja, Mikaya mwana wa Imla. Yeye twaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu. Lakini namchukia kwa sababu yeye kamwe hatabiri jambo jema juu yangu, ila mabaya tu.” Yehoshafati akamwambia, “Si vizuri mfalme kusema hivyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme wa Waisiraeli akamwambia Yosafati: Yuko bado mtu mmoja wa kumwuliza neno la Bwana, lakini mimi ninamchukia, kwani hanifumbulii yatakayokuwa mema, ila siku zote husema yatakayokuwa mabaya, naye ndiye Mikaya, mwana wa Imula. Yosafati akasema: Mfalme asiseme hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza BWANA kwa yeye; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme wa Israeli akamujibu Yosafati: “Kungali mumoja, Mikaya mwana wa Imula. Yeye tunaweza kumwuliza shauri la Yawe. Lakini ninamuchukia sana kwa sababu yeye hatabiri jambo jema juu yangu hata kidogo, lakini mabaya tu.” Yosafati akamwambia: “Si vizuri kwa mufalme kusema hivyo.”