2 Chronicles 19:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mara ndugu zenu kutoka katika mji wowote ule wanapowaletea shtaka lolote kuhusu uuaji, uvunjaji wa sheria, amri, kanuni au maagizo, washaurini vema ili wasije wakamkosea Mwenyezi-Mungu. Msipofanya hivyo, nyinyi pamoja na ndugu zenu mtapatwa na ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Lakini mkiutekeleza wajibu wenu, hamtakuwa na hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine kuhusu sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Mwenyezi Mungu, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, mtawaonya, wasiingie hatiani mbele za Bwana, mkajiliwa na ghadhabu ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mara ndugu zenu kutoka katika mji wowote ule wanapowaletea shtaka lolote kuhusu uuaji, uvunjaji wa sheria, amri, kanuni au maagizo, washaurini vema ili wasije wakamkosea Mwenyezi-Mungu. Msipofanya hivyo, nyinyi pamoja na ndugu zenu mtapatwa na ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Lakini mkiutekeleza wajibu wenu, hamtakuwa na hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasitende dhambi dhidi ya BWANA, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya bwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila mara watakapowaletea shitaka toka ndugu zenu wakaao mijini mwao, kuhusu uuaji, uvunjaji wa sheria na amri, kanuni au maagizo, mtawaonya, wasiingie hatiani mbele za BWANA, mkajiliwa na ghadhabu ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mara ndugu zenu kutoka katika mji wowote ule wanapowaletea shtaka lolote kuhusu uuaji, uvunjaji wa sheria, amri, kanuni au maagizo, washaurini vema ili wasije wakamkosea Mwenyezi-Mungu. Msipofanya hivyo, nyinyi pamoja na ndugu zenu mtapatwa na ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Lakini mkiutekeleza wajibu wenu, hamtakuwa na hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika magomvi yote yatakayoletwa kwenu na ndugu zenu wanaokaa katika miji yao, kama ni kugombeana damu zilizomwagwa au maonyo na maagizo au maongozi na maamuzi, mtawafundisha, wasimkosee Bwana, makali yakawajia ninyi nao walio ndugu zenu. Fanyeni hivyo, msikore manza!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, mtawaonya, wasiingie hatiani mbele za BWANA, mkajiliwa na ghadhabu ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara wandugu zenu kutoka katika muji wowote wanapowaletea mashitaki yoyote juu ya uuaji, kuvunja Sheria, amri, kanuni au maagizo, muwashaurie vema kusudi wasimukosee Yawe. Musipofanya hivyo, ninyi pamoja na wandugu zenu mutapatwa na kasirani ya Yawe. Lakini mukitenda vile, hamutakuwa na kosa.