2 Chronicles 19:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amaria, kuhani mkuu, ndiye atakayesimamia mambo yote yanayomhusu Mwenyezi-Mungu, naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, gavana wa Yuda atasimamia mambo yote ya utawala, na Walawi watakuwa maofisa. Jipeni moyo muyatekeleze masharti haya, naye Mwenyezi-Mungu awe pamoja nao walio wema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Mwenyezi Mungu naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yu juu yenu kwa maneno yote ya Bwana; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli, jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa maneno yote ya mfalme; Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye Bwana awe pamoja nao walio wema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amaria, kuhani mkuu, ndiye atakayesimamia mambo yote yanayomhusu Mwenyezi-Mungu, naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, gavana wa Yuda atasimamia mambo yote ya utawala, na Walawi watakuwa maofisa. Jipeni moyo muyatekeleze masharti haya, naye Mwenyezi-Mungu awe pamoja nao walio wema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Amaria Kuhani Mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lo lote linalomhusu BWANA naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kuhusiana na jambo lo lote la mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye BWANA atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu bwana naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye bwana atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yuko juu yenu kwa maneno yote ya BWANA; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli, jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa mambo yote ya mfalme; Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye BWANA awe pamoja nao walio wema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amaria, kuhani mkuu, ndiye atakayesimamia mambo yote yanayomhusu Mwenyezi-Mungu, naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, gavana wa Yuda atasimamia mambo yote ya utawala, na Walawi watakuwa maofisa. Jipeni moyo muyatekeleze masharti haya, naye Mwenyezi-Mungu awe pamoja nao walio wema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, mtambikaji mkuu Amaria atawaongoza katika mambo yote ya Bwana, naye Zebadia, mwana wa Isimaeli, mwenye amri wa mlango wa Yuda, atawaongoza katika mambo yote ya mfalme, nao Walawi wako mbele yenu kuwasimamia watu. Jipeni mioyo, kafanyeni hivyo! Ndipo, Bwana atakapokuwa nao wale walio wema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yu juu yenu kwa maneno yote ya BWANA; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli, jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa maneno yote ya mfalme; Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye BWANA awe pamoja nao walio wema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amaria, Kuhani Mukubwa, ndiye atakayesimamia mambo yote yanayoelekea Yawe, naye Zebadia mwana wa Isimaeli, musimamizi wa inchi ya Yuda atasimamia mambo yote ya utawala, na Walawi watakuwa wakubwa. Mujipe moyo mutimize masharti haya, naye Yawe akuwe pamoja nao wanaokuwa wema.”