2 Chronicles 19:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sasa mwogopeni Mwenyezi-Mungu, muwe waangalifu katika kila jambo mtakalotenda kwa sababu Mwenyezi-Mungu wetu hatavumilia upotoshaji wa haki, wala upendeleo wala ulaji rushwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi sasa kicho cha Mwenyezi Mungu na kiwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hakuna jambo la dhuluma, wala upendeleo, wala rushwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sasa mwogopeni Mwenyezi-Mungu, muwe waangalifu katika kila jambo mtakalotenda kwa sababu Mwenyezi-Mungu wetu hatavumilia upotoshaji wa haki, wala upendeleo wala ulaji rushwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa BWANA Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo wala rushwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi sasa hofu ya bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa bwana Mwenyezi Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; iweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sasa mwogopeni Mwenyezi-Mungu, muwe waangalifu katika kila jambo mtakalotenda kwa sababu Mwenyezi-Mungu wetu hatavumilia upotoshaji wa haki, wala upendeleo wala ulaji rushwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii tisho la Bwana na liwakalie, mzifanye kazi zenu na kujiangalia! Kwani kwake Bwana hakuna wala upotovu, wala upendeleo, wala upenyezi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sasa mumwogope Yawe, mukuwe waangalifu katika kila jambo mutakalotenda kwa sababu Yawe wetu hatavumilia upotoshaji wa haki, wala upendeleo wala upokeaji wa kituliro.”