2 Chronicles 19:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mjini Yerusalemu, Yehoshafati aliteua Walawi kadhaa, waamuzi na baadhi ya wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi wa magomvi yahusuyo uvunjaji wa sheria za Mwenyezi-Mungu, au ugomvi baina ya wakazi wa mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akasimamisha wa Walawi na makuhani, na wakuu wa mbari za mababa wa Israeli wawe kwa hukumu ya Bwana, na kwa mateto. Nao wakarudi Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mjini Yerusalemu, Yehoshafati aliteua Walawi kadhaa, waamuzi na baadhi ya wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi wa magomvi yahusuyo uvunjaji wa sheria za Mwenyezi-Mungu, au ugomvi baina ya wakazi wa mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya BWANA na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya bwana na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi kwa hukumu za BWANA na kesi kati yao. Nao wakarudi Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mjini Yerusalemu, Yehoshafati aliteua Walawi kadhaa, waamuzi na baadhi ya wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi wa magomvi yahusuyo uvunjaji wa sheria za Mwenyezi-Mungu, au ugomvi baina ya wakazi wa mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo Yerusalemu Yosafati akaweka Walawi wengine na watambikaji, hata wakuu wengine wa milango ya Isiraeli kumfanyizia Bwana kazi ya uamuzi na kuwagombea watu. Waliporudi Yerusalemu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akasimamisha wa Walawi na makuhani, na wakuu wa mbari za mababa wa Israeli wawe kwa hukumu ya BWANA, na kwa mateto. Nao wakarudi Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika muji wa Yerusalema, Yosafati akaweka Walawi makuhani na wakubwa wa jamaa za Waisraeli wakuwe waamuzi wa magomvi yanayoelekea sheria za Yawe, au ugomvi kati ya wakaaji wa muji.