2 Chronicles 2:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa ajili ya watumishi wako, yaani maseremala watakaopasua mbao, nitatoa tani 2,000 za ngano iliyopondwa, tani 2,000 za shayiri, lita 400,000 za divai na lita 400,000 za mafuta.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawapa watumishi wako, yaani maseremala wakatao mbao, kori elfu ishirini za unga wa ngano, kori elfu ishirini za shayiri, bathi elfu ishirini za mvinyo, na bathi elfu ishirini za mafuta ya zeituni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, nitawapa watumishi wako, wachongaji wakatao miti, kori
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa ajili ya watumishi wako, yaani maseremala watakaopasua mbao, nitatoa tani 2,000 za ngano iliyopondwa, tani 2,000 za shayiri, lita 400,000 za divai na lita 400,000 za mafuta.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000 za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000 za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,000 za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,000 za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, nitawapa watumishi wako, wachongaji wakatao miti, kori elfu ishirini za ngano iliyopondwa, na kori elfu ishirini za shayiri, na bathi elfu ishirini za mvinyo na bathi elfu ishirini za mafuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa ajili ya watumishi wako, yaani maseremala watakaopasua mbao, nitatoa tani 2,000 za ngano iliyopondwa, tani 2,000 za shayiri, lita 400,000 za divai na lita 400,000 za mafuta.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, maseremala wanaoichonga miti walio watu wako nitawapa kori 20000, ndio frasila 200000 za ngano na kori 20000, ndio frasila 200000 za mawele na bati 20000, ndio vibaba 700000 vya mvinyo na bati 20000, ndio vibaba 700000 vya mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, nitawapa watumishi wako, wachongaji wakatao miti, kori ishirini elfu za ngano iliyopondwa, na kori ishirini elfu za shayiri, na bathi ishirini elfu za mvinyo na bathi ishirini elfu za mafuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Hiramu, mufalme wa Tiro, akamujibu Solomono kwa barua akisema: “Kwa sababu Yawe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mufalme wao.