2 Chronicles 2:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia! Amempa mfalme Daudi mwana mwenye hekima, busara na akili, atakayemjengea Mwenyezi-Mungu nyumba, na kujijengea ikulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na busara, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee Bwana nyumba, na nyumba kwa ufalme wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia! Amempa mfalme Daudi mwana mwenye hekima, busara na akili, atakayemjengea Mwenyezi-Mungu nyumba, na kujijengea ikulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya BWANA, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee BWANA nyumba, na nyumba ya ufalme wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia! Amempa mfalme Daudi mwana mwenye hekima, busara na akili, atakayemjengea Mwenyezi-Mungu nyumba, na kujijengea ikulu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huramu akaendelea akisema: Bwana Mungu wa Isiraeli aliyeziumba mbingu na nchi na atukuzwe, kwa kuwa amempa mfalme Dawidi mwana aliye mwerevu wa kweli ajuaye kuzitumia akili na utambuzi, amjengee Bwana nyumba, ajijengee naye nyumba ya kifalme!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee BWANA nyumba, na nyumba kwa ufalme wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa ninakutumia fundi mwenye ujuzi sana na mwenye akili, jina lake Huruma-Abi.