2 Chronicles 2:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Solomoni aliamuru sensa ifanywe ya wageni wote walioishi katika nchi ya Israeli. Sensa hii ni kama ile aliyoifanya Daudi, baba yake. Kulikuwa na wageni wapatao 153,600.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Sulemani akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu elfu mia moja hamsini na tatu na mia sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, sawasawa na hesabu aliyowahesabu Daudi baba yake; wakatokea mia hamsini na tatu elfu, na mia sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Solomoni aliamuru sensa ifanywe ya wageni wote walioishi katika nchi ya Israeli. Sensa hii ni kama ile aliyoifanya Daudi, baba yake. Kulikuwa na wageni wapatao 153,600.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Solomoni akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu 153,600.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Sulemani akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu 153,600.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, kulingana na hesabu aliyoifanya Daudi baba yake; wakatokea elfu mia moja hamsini na tatu, na mia sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Solomoni aliamuru sensa ifanywe ya wageni wote walioishi katika nchi ya Israeli. Sensa hii ni kama ile aliyoifanya Daudi, baba yake. Kulikuwa na wageni wapatao 153,600.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Salomo alipowahesabu waume wageni wote waliokaa katika nchi, akiifuata njia ya kuhesabu, baba yake Dawidi aliyoishika alipowahesabu, wakaonekana watu 153600.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, sawasawa na hesabu aliyowahesabu Daudi baba yake; wakatokea mia hamsini na tatu elfu, na mia sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati yao akawapa watu elfu makumi saba kazi ya kubeba mizigo, watu elfu moja wakakuwa wachongaji wa mawe kwenye milima, na watu elfu tatu mia sita wakakuwa wasimamizi kusudi wawasukume watu kufanya kazi.