2 Chronicles 2:18 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati yao, 70,000 aliwapa kazi ya upagazi, 80,000 wakawa wachonga mawe milimani, na 3,600 wakawa wasimamizi ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaweka watu elfu sabini miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na elfu themanini kuwa wachonga mawe vilimani, na elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaweka katika hao sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na themanini elfu wawe wachongaji milimani, na wasimamizi elfu tatu na mia sita, ili wawatie watu kazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati yao, 70,000 aliwapa kazi ya upagazi, 80,000 wakawa wachonga mawe milimani, na 3,600 wakawa wasimamizi ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaweka watu 70,000 miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na 3,600 wakiwa wasimamizi juu yao ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaweka watu 70,000 miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na 3,600 wakiwa wasimamizi juu yao ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika hao akawaweka elfu sabini wawe wapagazi na elfu themanini wawe wachonga mawe milimani, na elfu tatu na mia sita wewe wasimamizi ili wawahimize watu kazini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati yao, 70,000 aliwapa kazi ya upagazi, 80,000 wakawa wachonga mawe milimani, na 3,600 wakawa wasimamizi ili wawahimize watu kufanya kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao hao akatoa 70000 kuwa wachukuzi, 80000 kuchonga mawe milimani, 3600 kuwa wasimamizi wa kuwafanyisha watu kazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaweka katika hao sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na themanini elfu wawe wachongaji milimani, na wasimamizi elfu tatu na mia sita, ili wawatie watu kazini.