2 Chronicles 2:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mwerezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akatuma watu kwa Hiramu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: “Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akatuma watu kwa Hiramu mfalme wa Tiro, akisema, Kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi, ajijengee nyumba ya kukaa, unitendee na mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Solomoni akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, akamwambia, “Nitendee na mimi kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, ulipompelekea mierezi ya kujengea ikulu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Salomo akatuma watu kwa Huramu, mfalme wa Tiro, kwamba: Kwa hivyo, ulivyopatana na baba yangu Dawidi, ukampelekea miti ya miangati ya kujijengea nyumba ya kukaa humo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akatuma watu kwa Hiramu mfalme wa Tiro, akisema, Kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi, ajijengee nyumba ya kukaa, unitendee na mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninataka kujenga nyumba ya kumwabudia Yawe wangu. Nitaitakasa kwa ajili yake, nayo itakuwa pahali pa kufukiza ubani wenye harufu nzuri mbele yake, na vilevile pahali pa kumutolea mikate mitakatifu siku zote, na sadaka za kuteketezwa asubui na magaribi na za siku za Sabato, za Mwandamo wa Mwezi, na sikukuu zingine za Yawe, Mungu wetu, kama vile alivyoagiza Waisraeli milele.