2 Chronicles 2:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama, karibu nianze kujenga nyumba ya kumwabudia Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Nitaiweka wakfu, nayo itakuwa mahali pa kufukiza ubani wa harufu nzuri mbele yake, na mahali pa mikate ya kuwekwa mbele yake daima, na tambiko za kuteketezwa asubuhi na jioni na pia siku za Sabato, mwezi mwandamo, na sikukuu nyinginezo za Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyoiagiza Israeli milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia, najenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za Bwana, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama, karibu nianze kujenga nyumba ya kumwabudia Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Nitaiweka wakfu, nayo itakuwa mahali pa kufukiza ubani wa harufu nzuri mbele yake, na mahali pa mikate ya kuwekwa mbele yake daima, na tambiko za kuteketezwa asubuhi na jioni na pia siku za Sabato, mwezi mwandamo, na sikukuu nyinginezo za Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyoiagiza Israeli milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la BWANA Mungu wangu na kuliweka wakfu kwake kwa ajili yakufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate Mitakatifu kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamuriwa za BWANA Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la bwana Mwenyezi Mungu wangu na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonyesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za bwana Mwenyezi Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia, najenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za BWANA, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama, karibu nianze kujenga nyumba ya kumwabudia Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Nitaiweka wakfu, nayo itakuwa mahali pa kufukiza ubani wa harufu nzuri mbele yake, na mahali pa mikate ya kuwekwa mbele yake daima, na tambiko za kuteketezwa asubuhi na jioni na pia siku za Sabato, mwezi mwandamo, na sikukuu nyinginezo za Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyoiagiza Israeli milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tazama, mimi ninataka kulijengea Jina la Bwana Mungu wangu nyumba, niitakase kuwa yake, wavukizie mle mbele yake mavukizo yanukayo vizuri, tena wamwekee mikate siku zote, tena wamtolee ng'ombe za tambiko za asubuhi na za jioni na za siku za mapumziko na za miandamo ya mwezi na za sikukuu za Bwana Mungu wetu, maana hayo ndiyo mazoeo ya Waisiraeli ya kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia, najenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za BWANA, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyumba ninayokusudia kujenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mukubwa zaidi ya miungu yote.