2 Chronicles 2:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba ikiwa mbingu zenyewe hazimtoshi, wala mbingu za juu sana? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba isipokuwa tu kama mahali pa kufukizia ubani mbele yake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele zake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba ikiwa mbingu zenyewe hazimtoshi, wala mbingu za juu sana? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba isipokuwa tu kama mahali pa kufukizia ubani mbele yake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, hazimtoshi? Mimi ni nani basi hata nijenge Hekalu kwa ajili yake, isipokuwa liwe tu kama mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya mahali pa kufukizia mafusho mbele zake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba ikiwa mbingu zenyewe hazimtoshi, wala mbingu za juu sana? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba isipokuwa tu kama mahali pa kufukizia ubani mbele yake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yuko nani anayejipatia nguvu ya kumjengea nyumba? Kwani haenei mbinguni, wala mbinguni palipo juu ya mbingu. Mimi nami ni mtu gani nikimjengea nyumba, isipokuwa ya kuvukizia tu mbele yake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele zake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sasa unitumie mutu mwenye ujuzi wa kutengeneza vyombo kwa zahabu, feza, shaba, na chuma, na nguo ya rangi nyekundu-nyeusi, za rangi nyekundu na ya samawi, anayejua vilevile kuchora. Yeye atashirikiana katika kazi hiyo na wafundi wanaokuwa pamoja nami katika Yuda na Yerusalema, ambao baba yangu Daudi aliwaweka.