2 Chronicles 20:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Shamu tokea ng’ambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ng'ambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako toka Edomu na ng'ambo ya Bahari. Tayari wako Hasason-Tamari” (ndio En-Gedi).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Edomu tokea ng’ambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio Engedi).
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wakaja kumpasha Yosafati habari kwamba: Uvumi wa watu wengi unakujia, unatoka ng'ambo ya huko ya bahari upande wa Ushami, nao wamekwisha kufika Hasesoni-Tamari, ndio Engedi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng’ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja wakakuja kumwambia mufalme Yosafati: “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha kufika Hazazoni-Tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi).