2 Chronicles 20:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake, wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda mpaka katika jangwa la Tekoa. Walipokuwa wanaondoka, Yehoshafati alisimama, akawaambia, “Nisikilizeni, enyi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu! Mwaminini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtakuwa imara. Muwe na imani na manabii wake, nanyi mtafaulu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake, wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda mpaka katika jangwa la Tekoa. Walipokuwa wanaondoka, Yehoshafati alisimama, akawaambia, “Nisikilizeni, enyi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu! Mwaminini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtakuwa imara. Muwe na imani na manabii wake, nanyi mtafaulu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, nanyi watu wa Yerusalemu! Mwaminini BWANA Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini bwana Mwenyezi Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake, wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda mpaka katika jangwa la Tekoa. Walipokuwa wanaondoka, Yehoshafati alisimama, akawaambia, “Nisikilizeni, enyi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu! Mwaminini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtakuwa imara. Muwe na imani na manabii wake, nanyi mtafaulu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake wakaondoka na mapema kwenda nyikani kwa Tekoa; hapo, walipotoka, Yosafati akasimama hapo akisema: Nisikilizeni, ninyi Wayuda na wenyeji wa Yerusalemu! Mtegemeeni Bwana Mungu wenu, ndipo, mtakaposhupazwa! Wategemeeni nao wafumbuaji wake, ndipo, mtakapofanikiwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake, wakaamuka asubui mapema, wakaenda mpaka katika jangwa la Tekoa. Walipokuwa wanaondoka, Yosafati akasimama, akawaambia: “Musikilize, enyi watu wa Yuda na wakaaji wa Yerusalema! Mumwamini Yawe, Mungu wenu, nanyi mutakuwa imara. Muwaaminie manabii wake, nanyi mutashinda.”