2 Chronicles 20:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kushauriana na watu, mfalme alichagua wanamuziki fulani, akawaagiza wajivike mavazi yao rasmi kisha watangulie mbele ya jeshi, wakiimba: “Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, maana fadhili zake zadumu milele!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa kuwa fadhili zake zadumu milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kushauriana na watu, mfalme alichagua wanamuziki fulani, akawaagiza wajivike mavazi yao rasmi kisha watangulie mbele ya jeshi, wakiimba: “Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, maana fadhili zake zadumu milele!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia BWANA na kumsifu katika uzuri wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni BWANA kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia bwana na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni bwana kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kushauriana na watu, mfalme alichagua wanamuziki fulani, akawaagiza wajivike mavazi yao rasmi kisha watangulie mbele ya jeshi, wakiimba: “Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, maana fadhili zake zadumu milele!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuwapa watu shauri hili akaweka watakaomwimbia Bwana nao watakaoutukuza urembo wa Patakatifu, watoke na kuwatangulia wenye mata na kusema: Mshukuruni Bwana, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya kushauriana na watu, mufalme akachagua waimbaji kwa kumwimbia Yawe wavae nguo zao takatifu kisha watangulie mbele ya jeshi, wakiimba: “Mumushukuru Yawe, maana wema wake unadumu milele!”