2 Chronicles 20:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Amoni na wa Moabu wakawashambulia wenyeji wa mlima Seiri, na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kuwaangamiza wakazi wa mlima Seiri wakaanza kushambuliana wao kwa wao, wakaangamizana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakaangamizana wao kwa wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Amoni na wa Moabu wakawashambulia wenyeji wa mlima Seiri, na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kuwaangamiza wakazi wa mlima Seiri wakaanza kushambuliana wao kwa wao, wakaangamizana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakasaidia kuangamizana wao kwa wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakaangamizana wao kwa wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwashambulia wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakaanza kuuana wao kwa wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Amoni na wa Moabu wakawashambulia wenyeji wa mlima Seiri, na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kuwaangamiza wakazi wa mlima Seiri wakaanza kushambuliana wao kwa wao, wakaangamizana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana wana wa Amoni na wa Moabu wakawainukia wenyeji wa milimani kwa Seiri na kuwaua na kuwaangamiza, walipokwisha kuwamaliza wenyeji wa Seiri, wakasaidiana kila mtu na mwenzake kuuana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamoni na Wamoabu wakawashambulia wenyeji wa mulima Seiri, na kuwaangamiza kabisa. Kisha kuwaangamiza wakaaji wa mulima Seiri wakaanza kushambuliana wao kwa wao, wakaangamizana.