2 Chronicles 20:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehoshafati na wanajeshi wake wakaenda kuchukua nyara wakakuta ng'ombe wengi, mali, nguo na vitu vingine vya thamani. Iliwachukua muda wa siku tatu kusomba nyara hizo, na hata hivyo, hawakuzimaliza kwani zilikuwa nyingi mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, mavazi na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehoshafati na wanajeshi wake wakaenda kuchukua nyara wakakuta ng'ombe wengi, mali, nguo na vitu vingine vya thamani. Iliwachukua muda wa siku tatu kusomba nyara hizo, na hata hivyo, hawakuzimaliza kwani zilikuwa nyingi mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, nguo na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, nguo na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nae Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakakuta miongoni mwao mifugo wengi sana, mali, mavazi na vitu vya thamani, walivyojinyakulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehoshafati na wanajeshi wake wakaenda kuchukua nyara wakakuta ng'ombe wengi, mali, nguo na vitu vingine vya thamani. Iliwachukua muda wa siku tatu kusomba nyara hizo, na hata hivyo, hawakuzimaliza kwani zilikuwa nyingi mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yosafati na watu wake walipokuja kujichukulia nyara, wakaona kwao mali nyingi penye hiyo mizoga na vyombo vyenye kima, wakawavua vingi mno, wasiweze kuvichikua vyote; wakawako siku tatu wakipokonya nyara, kwani zilikuwa nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosafati na waaskari wake wakaenda kukamata vitu. Wakakuta ngombe wengi, mali, nguo na vitu vingine vya bei kali. Iliwachukua muda wa siku tatu kusomba vitu hivyo, na hata hivyo, hawakuvimaliza maana vilikuwa vingi sana.