2 Chronicles 20:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Sifa, na kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa yote aliyowafanyia. Ndio maana bonde hilo linaitwa Bonde la Sifa hadi hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka, mahali walikomtukuza Mwenyezi Mungu. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Sifa, na kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa yote aliyowafanyia. Ndio maana bonde hilo linaitwa Bonde la Sifa hadi hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka kwa maana huko ndiko walikomsifu BWANA. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka mpaka leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka kwa maana huko ndiko walikomsifu bwana. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka mpaka leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipomtukuza BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Sifa, na kumsifu Mwenyezi-Mungu kwa yote aliyowafanyia. Ndio maana bonde hilo linaitwa Bonde la Sifa hadi hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Tukuzo, kwani huko ndiko, walikomtukuzia Bwana; kwa sababu hii mahali pale wakapaita Bonde la Tukuzo hata leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya ine wakakusanyika katika Bonde la Sifa, na kumusifu Yawe kwa yote aliyowafanyia. Hii ndiyo sababu bonde hilo linaitwa Bonde la Sifa mpaka hivi leo.