2 Chronicles 20:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yehoshafati akawaongoza wanajeshi wake mpaka Yerusalemu kwa shangwe, kwa sababu Mwenyezi-Mungu aliwashinda maadui zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wanaume wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yehoshafati akawaongoza wanajeshi wake mpaka Yerusalemu kwa shangwe, kwa sababu Mwenyezi-Mungu aliwashinda maadui zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kwa kuwa BWANA alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kwa kuwa bwana alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa BWANA amewafurahisha juu ya adui zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yehoshafati akawaongoza wanajeshi wake mpaka Yerusalemu kwa shangwe, kwa sababu Mwenyezi-Mungu aliwashinda maadui zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watu wote wa Yuda na wa Yerusalemu wakarudi, naye Yosafati akawatangulia kurudi Yerusalemu na kufurahi, kwani Bwana aliwapa kuwafurahia adui zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa BWANA amewafurahisha juu ya adui zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yosafati akawaongoza waaskari wake mpaka Yerusalema kwa shangwe, kwa sababu Yawe aliwashinda waadui zao.