2 Chronicles 20:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akaomba kwa sauti akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu, wewe ndiwe Mungu uliye mbinguni! Wewe unazitawala falme zote duniani; unao uwezo na nguvu, wala hakuna awezaye kukupinga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akasema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe unayetawala juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna yeyote anayeweza kushindana nawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akaomba kwa sauti akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu, wewe ndiwe Mungu uliye mbinguni! Wewe unazitawala falme zote duniani; unao uwezo na nguvu, wala hakuna awezaye kukupinga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akasema: “Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe utawalaye juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna ye yote awezaye kushindana nawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akasema: “Ee bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe utawalaye juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna yeyote awezaye kushindana nawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akaomba kwa sauti akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu, wewe ndiwe Mungu uliye mbinguni! Wewe unazitawala falme zote duniani; unao uwezo na nguvu, wala hakuna awezaye kukupinga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Bwana Mungu wa baba zetu, wewe siwe Mungu akaaye mbinguni na kuzitawala nchi zote za wamizimu zenye wafalme? Mkononi mwako zimo nguvu na uwezo mwingi, hakuna awezaye kujisimamisha kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akaomba kwa sauti akisema: “Ee Yawe, Mungu wa babu zetu, wewe ndiwe Mungu unayekuwa mbinguni! Wewe unatawala falme zote katika dunia, una uwezo na nguvu, wala hakuna anayeweza kukupinga.