2 Chronicles 21:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo Edomu imeuasi utawala wa Yuda mpaka sasa. Wakati huohuo pia, wakazi wa Libna nao wakauasi utawala wake kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo Edomu imeuasi utawala wa Yuda mpaka sasa. Wakati huohuo pia, wakazi wa Libna nao wakauasi utawala wake kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hadi leo Edomu imeasi Yuda. Libna nao wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha bwana, Mungu wa baba zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo Edomu wakaasi utawala wa Yuda hata leo; wakati huo huo, Libna nao wakaasi utawala wake, kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo Edomu imeuasi utawala wa Yuda mpaka sasa. Wakati huohuo pia, wakazi wa Libna nao wakauasi utawala wake kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Waedomu wakalivunja agano tena, wakajitoa mikononi mwa Wayuda mpaka siku hii ya leo. Siku zile ndipo, nao wa Libuna walipolivunja agano na kujitoa mkononi mwake, kwani alimwacha Bwana Mungu wa baba zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo Waedomu wakaasi utawala wa Yuda mpaka sasa. Wakati uleule, vilevile wakaaji wa Libuna nao wakaasi utawala wake kwa sababu Yoramu alikuwa amemwacha Yawe, Mungu wa babu zake.