2 Chronicles 21:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehoramu alianza kutawala akiwa na umri wa miaka thelathini na miwili; akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka minane. Wakati alipofariki, hakuna mtu yeyote aliyemsikitikia. Alizikwa katika mji wa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka nane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehoramu alianza kutawala akiwa na umri wa miaka thelathini na miwili; akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka minane. Wakati alipofariki, hakuna mtu yeyote aliyemsikitikia. Alizikwa katika mji wa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu ye yote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehoramu alianza kutawala akiwa na umri wa miaka thelathini na miwili; akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka minane. Wakati alipofariki, hakuna mtu yeyote aliyemsikitikia. Alizikwa katika mji wa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alikuwa mwenye miaka 32 alipoupata ufalme, akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 8, akajiendea pasipo kuombolezewa, wakamzika mjini mwa Dawidi, lakini hawakumzika makaburini kwa wafalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoramu alianza kutawala akiwa na umri wa miaka makumi tatu na miwili; akatawala kule Yerusalema kwa muda wa miaka minane. Wakati alipokufa, hakuna mutu yeyote aliyemusikitikia. Alizikwa katika muji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.