2 Chronicles 21:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba yao aliwapa zawadi kubwakubwa za fedha, dhahabu na vitu vingine vya thamani, na pia miji ya Yuda yenye ngome. Lakini kwa sababu Yehoramu ndiye aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza, Yehoshafati akampa ufalme atawale badala yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali akampa Yehoramu ufalme kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, na za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba yao aliwapa zawadi kubwakubwa za fedha, dhahabu na vitu vingine vya thamani, na pia miji ya Yuda yenye ngome. Lakini kwa sababu Yehoramu ndiye aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza, Yehoshafati akampa ufalme atawale badala yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba yao aliwapa zawadi kubwakubwa za fedha, dhahabu na vitu vingine vya thamani, na pia miji ya Yuda yenye ngome. Lakini kwa sababu Yehoramu ndiye aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza, Yehoshafati akampa ufalme atawale badala yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa baba yao aliwapa vipaji vingi vya fedha na vya dhahabu na vya vitu vyenye kima, pamoja na miji yenye maboma katika nchi ya Yuda, lakini ufalme alimpa Yoramu, kwani huyu alikuwa mwanawe kwa kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, na za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baba yao aliwapa zawadi kubwakubwa za feza, zahabu na vitu vingine vya bei kali, na vilevile miji ya Yuda yenye kuta. Lakini kwa sababu Yoramu ndiye aliyekuwa muzaliwa wake wa kwanza, Yosafati akamupa ufalme atawale kwa pahali pake.