2 Chronicles 21:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini Mwenyezi-Mungu hakutaka kuangamiza ukoo wa Daudi kwa ajili ya agano alilokuwa amefanya na Daudi na pia kwa sababu alikuwa ameahidi wazawa wake wataendelea kutawala milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, kwa sababu ya agano ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amefanya na Daudi, Mwenyezi Mungu hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini Bwana hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini Mwenyezi-Mungu hakutaka kuangamiza ukoo wa Daudi kwa ajili ya agano alilokuwa amefanya na Daudi na pia kwa sababu alikuwa ameahidi wazawa wake wataendelea kutawala milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo BWANA alikuwa amefanya na Daudi, BWANA hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi, Mungu alikuwa ameahidi kumpa Daudi taa, yeye na wazao wake milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo bwana alikuwa amefanya na Daudi, bwana hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini Mwenyezi-Mungu hakutaka kuangamiza ukoo wa Daudi kwa ajili ya agano alilokuwa amefanya na Daudi na pia kwa sababu alikuwa ameahidi wazawa wake wataendelea kutawala milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana hakutaka kuuangamiza mlango wa Dawidi kwa ajili ya agano, alilolifanya na Dawidi, kwa kuwa alisema, ya kama atampa yeye na wanawe kuwa taa iwakayo siku zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini Yawe hakutaka kuangamiza ukoo wa Daudi kwa ajili ya agano alilokuwa amefanya na Daudi vilevile kwa sababu alikuwa ameahidi kwamba wazao wake wataendelea kutawala milele.