2 Chronicles 22:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu alimchukua Yoashi, akamtwaa kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Alimficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu, mke wa kuhani Yehoadani, kwa sababu alikuwa dadaye Ahazia, alimficha Yoashi ili Athalia asimuue.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yehosheba, binti Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila Yehosheba, binti mfalme, akamtwaa Yoashi, mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliouawa, akamweka yeye na yaya wake katika chumba cha kulala. Basi Yehosheba, binti mfalme Yehoramu, mkewe Yehoyada kuhani, (naye alikuwa umbu lake Ahazia,) akaficha usoni pa Athalia, asimwue.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu alimchukua Yoashi, akamtwaa kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Alimficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu, mke wa kuhani Yehoadani, kwa sababu alikuwa dadaye Ahazia, alimficha Yoashi ili Athalia asimuue.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia na kumwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa wanakaribia kuuawa. Akamweka yeye pamoja na yaya wake kwenye chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, mkewe Kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha mtoto ili Athalia asimwue.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti wa Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila Yehosheba, binti mfalme, akamtwaa Yoashi, mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa, akamweka yeye na yaya wake katika chumba cha kulala. Basi Yehosheba, binti mfalme Yehoramu, mkewe Yehoyada kuhani, (naye alikuwa dada yake Ahazia,) akamficha ili Athalia, asimwue.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu alimchukua Yoashi, akamtwaa kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Alimficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yehosheba, binti ya mfalme Yehoramu, mke wa kuhani Yehoadani, kwa sababu alikuwa dadaye Ahazia, alimficha Yoashi ili Athalia asimuue.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yosabati, binti mfalme, akamchukua Yoasi, mwana wa Ahazia, akamwiba katikati ya wana wa mfalme waliokwenda kuuawa, akamweka pamoja na mnyonyeshaji wake katika chumba cha kulalia. Ndivyo, Yosabati, binti mfalme Yoramu, mkewe mtambikaji Yoyada, aliyekuwa umbu lake Ahazia, alivyomficha Yoasi, Atalia asimwone, asipate kumwua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila Yehosheba, binti mfalme, akamtwaa Yoashi, mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliouawa, akamweka yeye na yaya wake katika chumba cha kulala. Basi Yehosheba, binti mfalme Yehoramu, mkewe Yehoyada kuhani, (naye alikuwa umbu lake Ahazia,) akaficha usoni pa Athalia, asimwue.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yoseba, binti ya mufalme Yoramu alimutwaa Yoasi, akamuchukua kwa siri kutoka kati ya wana wa mufalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamuficha yeye pamoja na yaya wake, katika chumba cha kulala. Hivyo Yoseba, binti ya mufalme Yoramu, muke wa kuhani Yoyada, kwa sababu alikuwa dada ya Ahazia, akamuficha Yoasi kusudi Atalia asimwone na kumwua.