2 Chronicles 22:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hiyo ilikuwa imepangwa na Mungu kuwa maangamizi yampate Ahazia kwa njia hiyo ya kumtembelea Yoramu. Maana alipofika huko, alitoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu mwana wa Nimshi ambaye Mwenyezi-Mungu alimteua kuuangamiza uzao wa Ahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu alisababisha anguko la Ahazia kutokana na Ahazia kwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Mwenyezi Mungu alikuwa amempaka mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Bwana alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hiyo ilikuwa imepangwa na Mungu kuwa maangamizi yampate Ahazia kwa njia hiyo ya kumtembelea Yoramu. Maana alipofika huko, alitoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu mwana wa Nimshi ambaye Mwenyezi-Mungu alimteua kuuangamiza uzao wa Ahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu alikuwa ameamuru kwamba kuanguka kwa Ahazia kungetokea atakapokwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alikuwa amemtia mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu alikuwa ameamuru kwamba kuanguka kwa Ahazia kungetokea atakapokwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye bwana alikuwa amemtia mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hiyo ilikuwa imepangwa na Mungu kuwa maangamizi yampate Ahazia kwa njia hiyo ya kumtembelea Yoramu. Maana alipofika huko, alitoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu mwana wa Nimshi ambaye Mwenyezi-Mungu alimteua kuuangamiza uzao wa Ahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili lilitoka kwake Mungu kuwa mwangamizo wake Ahazia, alipofika kwa Yoramu: kwani alipokwisha kufika akatoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu, mwana wa Nimusi, Bwana aliyempaka mafuta, aung'oe mlango wa Ahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ilikuwa imepangwa na Mungu kwamba maangamizi yatendeke kwa Ahazia kwa njia hiyo ya kumutembelea Yoramu; kwa sababu alipofika kule, alitoka pamoja na Yoramu kwenda kupigana na Yehu mwana wa Nimusi ambaye Yawe alimuchagua kwa kuangamiza uzao wa Ahabu.