2 Chronicles 22:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimtafuta Ahazia, naye akakamatwa akiwa amejificha huko Samaria. Walimleta hadi kwa Yehu, akauawa. Waliuzika mwili wake kwani walisema, “Yeye ni mjukuu wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote.” Hapakubaki hata mtu mmoja wa jamaa ya Ahazia ambaye angeweza kuwa falme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamuua. Wakamzika, kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Mwenyezi Mungu kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta Bwana kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimtafuta Ahazia, naye akakamatwa akiwa amejificha huko Samaria. Walimleta hadi kwa Yehu, akauawa. Waliuzika mwili wake kwani walisema, “Yeye ni mjukuu wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote.” Hapakubaki hata mtu mmoja wa jamaa ya Ahazia ambaye angeweza kuwa falme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamwua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta BWANA kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamuua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta bwana kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta BWANA kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alimtafuta Ahazia, naye akakamatwa akiwa amejificha huko Samaria. Walimleta hadi kwa Yehu, akauawa. Waliuzika mwili wake kwani walisema, “Yeye ni mjukuu wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote.” Hapakubaki hata mtu mmoja wa jamaa ya Ahazia ambaye angeweza kuwa falme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoagiza kumtafuta Ahazia, wakamkamatia Samaria, alikojificha, wakampeleka kwa Yehu, wakamwua, wakamzika, kwani walisema: Yeye ni mwana wa Yosafati aliyemtafuta Bwana kwa moyo wake wote. Lakini katika mlango wa Ahazia hakuwako mwenye nguvu aliyeweza kuwa mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta BWANA kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamutafuta Ahazia, naye akakamatwa akiwa amejificha kule Samaria. Wakamuleta mpaka kwa Yehu, akauawa. Wakauzika mwili wake maana walisema: “Yeye ni mujukuu wa Yosafati, ambaye alimutafuta Yawe kwa moyo wake wote.” Hapakubaki hata mutu mumoja wa jamaa ya Ahazia ambaye angeweza kushika ufalme.