2 Chronicles 23:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, mnamo mwaka wa saba, kuhani Yehoyada alijipa moyo akafanya mapatano na makapteni: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa saba, Yehoyada akaonesha nguvu zake. Alifanya agano na wakuu wa vikosi vya mamia: yaani Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mwaka wa saba Yehoyada akajitia nguvu, akawatwaa maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, mnamo mwaka wa saba, kuhani Yehoyada alijipa moyo akafanya mapatano na makapteni: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa saba Yehoyada akaonyesha nguvu zake. Akafanya agano na majemadari wa vikosi vya mamia: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa saba, Yehoyada akaonyesha nguvu zake. Alifanya agano na wakuu wa vikosi vya mamia: yaani Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa saba Yehoyada akajitia ujasiri, akawatwaa makamanda wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, mnamo mwaka wa saba, kuhani Yehoyada alijipa moyo akafanya mapatano na makapteni: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa saba Yoyada akajishupaza, akawachukua wakuu wa mamia, Azaria, mwana wa Yerohamu, na Isimaeli, mwana wa Yohana, na Azaria, mwana wa Obedi, na Masea, mwana wa Adaya, na Elisafati, mwana wa Zikiri, akafanya maagano nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mwaka wa saba Yehoyada akajitia nguvu, akawatwaa maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa saba kuhani Yoyada akajipa moyo akafanya mapatano na majemadari: Azaria mwana wa Yoramu, Isimaeli mwana wa Yohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maseya mwana wa Adaya, na Elisafati mwana wa Zikiri.