2 Chronicles 23:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu wakamtoa nje mwana wa mfalme, wakamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza nao Yehoyada na wanawe wakampaka mafuta awe mfalme, kisha watu wakashangilia wakisema, “Aishi mfalme!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyada na wanawe wakamtoa Yoashi mwana wa mfalme nje na kumvika taji. Wakampa nakala ya agano na kumtangaza kuwa mfalme. Wakampaka mafuta na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakamleta nje mwana wa mfalme, wakamvika taji, na kumpa ule ushuhuda, wakamtawaza awe mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu wakamtoa nje mwana wa mfalme, wakamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza nao Yehoyada na wanawe wakampaka mafuta awe mfalme, kisha watu wakashangilia wakisema, “Aishi mfalme!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoyada na wanawe wakamtoa nje Yoashi mwana wa mfalme nao wakamvika taji wakampa nakala ya Agano na kumtangaza kuwa mfalme. Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, nao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoyada na wanawe wakamtoa Yoashi mwana wa mfalme nje na kumvika taji. Wakampa nakala ya agano na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakamleta nje mwana wa mfalme, wakamvika taji, na kumpa ule ushuhuda, wakamtawaza kuwa mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu wakamtoa nje mwana wa mfalme, wakamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza nao Yehoyada na wanawe wakampaka mafuta awe mfalme, kisha watu wakashangilia wakisema, “Aishi mfalme!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakamtoa mwana wa mfalme, wakamvika kilemba cha kifalme, wakampa nacho kizingo cha Ushahidi, wakamfanya kuwa mfalme, Yoyada na wanawe wakimpaka mafuta na kusema: pongezi, mfalme!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakamleta nje mwana wa mfalme, wakamvika taji, na kumpa ule ushuhuda, wakamtawaza awe mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakamutoa mwana wa mufalme inje wakamuvalisha taji juu ya kichwa, na kumupa ule ushuhuda; wakamuweka kuwa mufalme nao Yoyada na wana wake wakamupakaa mafuta kisha watu wakashangilia wakisema: “Mufalme aishi milele!”