2 Chronicles 23:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipochungulia akamwona mfalme mpya amesimama karibu na nguzo kwenye lango, huku makapteni na wapiga tarumbeta wakiwa kando ya mfalme na wakazi wote wakishangilia na kupiga tarumbeta; nao waimbaji wakiwa na ala zao za muziki wakiongoza watu katika sherehe; ndipo aliporarua nguo zake na kusema kwa sauti kubwa “Uhaini! Uhaini!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaangalia, na tazama, mfalme alikuwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta, na waimbaji waliokuwa na vyombo vya uimbaji walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kulia, “Uhaini! Uhaini!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao maakida na wenye mapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga mapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Fitina! Fitina!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipochungulia akamwona mfalme mpya amesimama karibu na nguzo kwenye lango, huku makapteni na wapiga tarumbeta wakiwa kando ya mfalme na wakazi wote wakishangilia na kupiga tarumbeta; nao waimbaji wakiwa na ala zao za muziki wakiongoza watu katika sherehe; ndipo aliporarua nguo zake na kusema kwa sauti kubwa “Uhaini! Uhaini!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao makamanda na wenye parapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga parapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Uhaini! Uhaini!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipochungulia akamwona mfalme mpya amesimama karibu na nguzo kwenye lango, huku makapteni na wapiga tarumbeta wakiwa kando ya mfalme na wakazi wote wakishangilia na kupiga tarumbeta; nao waimbaji wakiwa na ala zao za muziki wakiongoza watu katika sherehe; ndipo aliporarua nguo zake na kusema kwa sauti kubwa “Uhaini! Uhaini!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipotazama, akamwona mfalme, akisimama katika ulingo wake pa kuingilia, nao wakuu na wapiga matarumbeta wakisimama kwake mfalme, nao watu wote wa nchi yao wakawa wenye furaha na kupiga matarumbeta, nao waimbaji wakavipiga vyombo vya kuimbia, wakawaongoza watu kushangilia. Ndipo, Atalia alipoyararua mavazi yake na kupiga kelele kwamba: Mmedanganyika! Mmedanganyika!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao maakida na wenye mapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga mapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Fitina! Fitina!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipochungulia akamwona mufalme mupya akisimama karibu na nguzo kwenye mulango, wakati majemadari na wapiga baragumu wakiwa kando ya mufalme na wakaaji wote wakishangilia na kupiga baragumu; nao waimbaji wakiwa na ala zao za muziki wakiongoza watu katika sherehe; halafu akapasua nguo yake na kusema kwa sauti kubwa: “Uasi! Uasi!”