2 Chronicles 23:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha kuhani Yehoyada aliwatoa nje makapteni wa jeshi akisema mtoeni nje katikati ya askari; yeyote atakayemfuata na auawe kwa upanga. Kwa sababu alisema “Msimuulie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani Yehoyada akawatuma majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, na kuwaambia: “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimuulie ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yehoyada kuhani akawaleta nje maakida wa mamia, waliowekwa juu ya jeshi, akawaambia, Mtoeni nje kati ya safu; naye ye yote amfuataye, na auawe kwa upanga; kwani kuhani amesema, Msimwue katika nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha kuhani Yehoyada aliwatoa nje makapteni wa jeshi akisema mtoeni nje katikati ya askari; yeyote atakayemfuata na auawe kwa upanga. Kwa sababu alisema “Msimuulie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani Yehoyada akawatoa nje majemadari wa vikosi vya mia, waliokuwa viongozi wa jeshi na kuwaambia: “Mtoeni nje kati ya safu na mkamwue kwa upanga ye yote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimwulie ndani ya Hekalu la BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani Yehoyada akawatuma majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, na kuwaambia: “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimuulie ndani ya Hekalu la bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yehoyada kuhani akawaleta nje makamanda wa mamia, waliowekwa kuongoza jeshi, akawaambia, Mtoeni nje kati ya safu; na yeyote amfuataye, na auawe kwa upanga; kwani kuhani amesema, Msimwue katika nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha kuhani Yehoyada aliwatoa nje makapteni wa jeshi akisema mtoeni nje katikati ya askari; yeyote atakayemfuata na auawe kwa upanga. Kwa sababu alisema “Msimuulie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji Yoyada alipowatoa wakuu wa mamia waliovisimamia vikosi, akawaambia: Mtoeni hapa penye mipango ya watu! Naye atakayemfuata na auawe kwa upanga! Kwani mtambikaji alisema: Msimwue Nyumbani mwa Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yehoyada kuhani akawaleta nje maakida wa mamia, waliowekwa juu ya jeshi, akawaambia, Mtoeni nje kati ya safu; naye ye yote amfuataye, na auawe kwa upanga; kwani kuhani amesema, Msimwue katika nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuhani Yoyada akawatoa inje majemadari wa jeshi akisema: “Mumutoe Atalia inje katikati ya waaskari; yeyote atakayemufuata auawe kwa upanga,” kwa sababu hakutaka wamwue katika nyumba ya Yawe.