2 Chronicles 23:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Hao walinzi walisimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika huduma ya kutunza nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu mikononi mwa makuhani, hao Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kushangilia na kuimba, vile Daudi alikuwa ameagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya Bwana chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa Bwana, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za Bwana, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Hao walinzi walisimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika huduma ya kutunza nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Kuhani Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la BWANA mikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za BWANA kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la bwana mikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za bwana kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Hao walinzi walisimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika huduma ya kutunza nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yoyada akaweka watambikaji na Walawi kuwa wakaguzi wa Nyumba ya Bwana, kwani Dawidi aliwapatia hao kazi ya kuiangalia Nyumba ya Bwana, wamteketezee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, kama ilivyoandikwa katika Maonyo ya Mose, pamoja na kuimba nyimbo za furaha, kama Dawidi alivyowaongoza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani Yoyada akaweka walinzi kwa kulinda nyumba ya Yawe. Hao walinzi wakasimamiwa na makuhani na Walawi ambao Daudi aliwaweka katika kazi ya kutunza nyumba ya Yawe kutoa sadaka za kutetezwa kwa moto kwa Yawe kama vile ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, wakishangilia na kuimba kwa kufuata amri ya Daudi. Vilevile wakasimamia mambo ya uimbaji na sherehe.