2 Chronicles 23:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwachukua makapteni wa jeshi, waheshimiwa, watawala wa watu, na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakapitia katika lango la juu mpaka ikulu. Kisha wakamkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Wakaingia kwenye jumba la mfalme kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha ufalme;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawatwaa maakida wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamtelemsha mfalme kutoka nyumba ya Bwana; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwachukua makapteni wa jeshi, waheshimiwa, watawala wa watu, na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakapitia katika lango la juu mpaka ikulu. Kisha wakamkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka hekaluni mwa BWANA. Wakaingia kwenye jumba la kifalme kwa kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi cha ufalme,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka Hekalu la bwana. Wakaingia kwenye jumba la mfalme kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawatwaa makamanda wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamteremsha mfalme kutoka nyumba ya BWANA; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwachukua makapteni wa jeshi, waheshimiwa, watawala wa watu, na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakapitia katika lango la juu mpaka ikulu. Kisha wakamkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawachukua wakuu wa mamia na watukufu na watawalaji wa watu nao watu wote wa nchi hii, akamtoa mfalme Nyumbani mwa Bwana, wakaingia nyumbani mwa mfalme na kupita katikati katika lango la juu, wakamketisha mfalme katika kiti cha kifalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawatwaa maakida wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamtelemsha mfalme kutoka nyumba ya BWANA; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitwaa majemadari wa jeshi, waheshimiwa, watawala wa watu, na wakaaji wote; nao wakamusindikiza mufalme kutoka nyumba ya Yawe, wakapitia katika mulango wa juu mpaka kwenye nyumba ya kifalme. Kisha wakamuikalisha mufalme kwenye kiti cha kifalme.