2 Chronicles 23:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
theluthi nyingine italinda ikulu na theluthi iliyobakia mtalinda Lango la Msingi. Watu wote watakuwa katika nyua za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
theluthi yenu mtalinda jumba la kifalme, na theluthi nyingine mtalinda Lango la Msingi. Walinzi wengine wote mwe ndani ya nyua za Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na theluthi nyumbani pa mfalme; na theluthi mlangoni pa msingi; na watu wote watakuwapo nyuani mwa nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
theluthi nyingine italinda ikulu na theluthi iliyobakia mtalinda Lango la Msingi. Watu wote watakuwa katika nyua za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
theluthi watalinda jumba la kifalme, theluthi nyingine watalinda Lango la Msingi. Watu wengine wote itawapasa wawe ndani ya nyua za Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
theluthi yenu mtalinda jumba la kifalme, na theluthi nyingine mtalinda Lango la Msingi. Walinzi wengine wote mwe ndani ya nyua za Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na theluthi nyumbani pa mfalme; na theluthi langoni pa msingi; na watu wote watakuwapo nyuani mwa nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
theluthi nyingine italinda ikulu na theluthi iliyobakia mtalinda Lango la Msingi. Watu wote watakuwa katika nyua za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
fungu jingine la tatu sharti walinde nyumbani mwa mfalme, fungu jingine la tatu walinde langoni penye msingi. Kisha watu wote waje nyuani penye Nyumba ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na theluthi nyumbani pa mfalme; na theluthi mlangoni pa msingi; na watu wote watakuwapo nyuani mwa nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
sehemu moja ya tatu ingine italinda nyumba ya kifalme na sehemu iliyobakia mutalinda Mulango wa Musingi. Watu wote watakuwa katika viwanja vya nyumba ya Yawe.