2 Chronicles 23:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asikubaliwe mtu mwingine yeyote kuingia nyumba ya Mwenyezi-Mungu isipokuwa makuhani tu pekee na wale Walawi watakaokuwa wanahudumu. Hao wanaweza kuingia kwa sababu wao ni watakatifu, lakini wale watu wengine wote, watatii amri ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna mtu yeyote ataingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu isipokuwa makuhani na Walawi walio kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kulinda kile walichoamriwa na Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala asiingie mtu nyumbani mwa Bwana, ila makuhani, na hao watumikao wa Walawi; hao wataingia, kwa kuwa hao ni watakatifu; ila watu wote watalinda malinzi ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asikubaliwe mtu mwingine yeyote kuingia nyumba ya Mwenyezi-Mungu isipokuwa makuhani tu pekee na wale Walawi watakaokuwa wanahudumu. Hao wanaweza kuingia kwa sababu wao ni watakatifu, lakini wale watu wengine wote, watatii amri ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna ruhusa mtu ye yote kuingia Hekaluni mwa BWANA isipokuwa makuhani na Walawi walioko kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kuangalia kile kilichoamriwa na BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna mtu yeyote ataingia katika Hekalu la bwana isipokuwa makuhani na Walawi walioko kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kulinda kile walichoamriwa na bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala asiingie mtu nyumbani mwa BWANA, ila makuhani, na Walawi watumikao; hao wataingia, kwa kuwa ni watakatifu; ila watu wengine wote watafuata amri za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asikubaliwe mtu mwingine yeyote kuingia nyumba ya Mwenyezi-Mungu isipokuwa makuhani tu pekee na wale Walawi watakaokuwa wanahudumu. Hao wanaweza kuingia kwa sababu wao ni watakatifu, lakini wale watu wengine wote, watatii amri ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Nyumbani mwa Bwana mtu asiingie, wasipokuwa watambikaji nao Walawi wanaotumikia. Hao wataingia, kwani ndio watakatifu. Nao watu wote sharti walinde ulinzi wa Bwana,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala asiingie mtu nyumbani mwa BWANA, ila makuhani, na hao watumikao wa Walawi; hao wataingia, kwa kuwa hao ni watakatifu; ila watu wote watalinda malinzi ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asikubaliwe mutu mwingine yeyote kuingia ndani ya nyumba ya Yawe isipokuwa makuhani tu pekee na wale Walawi watakaokuwa wanatumika. Hao wanaweza kuingia kwa sababu wao ni watakatifu, lakini wale watu wengine wote, watatii amri ya Yawe.