2 Chronicles 23:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha kuhani Yehoyada akawapa makapteni mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya mfalme Daudi, na ambazo zilikuwa zimewekwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kuhani Yehoyada akawapa wakuu wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yehoyada kuhani akawapa maakida wa mamia mikuki, na ngao, na vigao, vilivyokuwa vya mfalme Daudi, vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha kuhani Yehoyada akawapa makapteni mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya mfalme Daudi, na ambazo zilikuwa zimewekwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akawapa majemadari wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya Mfalme Daudi na ambazo zilikuwa ndani ya Hekalu la Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akawapa wakuu wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yehoyada kuhani akawapa makamanda wa mamia mikuki, na ngao, na vigao, vilivyokuwa vya mfalme Daudi, vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha kuhani Yehoyada akawapa makapteni mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya mfalme Daudi, na ambazo zilikuwa zimewekwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtambikaji Yoyada akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao ndogo na kubwa za mfalme Dawidi zilizokuwa Nyumbani mwa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yehoyada kuhani akawapa maakida wa mamia mikuki, na ngao, na vigao, vilivyokuwa vya mfalme Daudi, vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuhani Yoyada akawapa majemadari mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya mufalme Daudi, na ambazo zilikuwa zimewekwa katika nyumba ya Yawe.