2 Chronicles 24:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme na Yehoyada walizitoa fedha hizo na kuwapa wale waliosimamia kazi ya urekebishaji wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nao wakawaajiri waashi, maseremala warekebishe nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Waliajiri pia mafundi wa chuma na shaba ili kurekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la Mwenyezi Mungu, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya Bwana, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme na Yehoyada walizitoa fedha hizo na kuwapa wale waliosimamia kazi ya urekebishaji wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nao wakawaajiri waashi, maseremala warekebishe nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Waliajiri pia mafundi wa chuma na shaba ili kurekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la BWANA. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la BWANA, pia wafanya kazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la bwana. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la bwana, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme na Yehoyada walizitoa fedha hizo na kuwapa wale waliosimamia kazi ya urekebishaji wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nao wakawaajiri waashi, maseremala warekebishe nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Waliajiri pia mafundi wa chuma na shaba ili kurekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme na Yoyada wakawapa mafundi wa kazi za kuitengeneza Nyumba ya Bwana; nao wakajitafutia waashi na maseremala wa kuirudishia Nyumba ya Bwana upya, hata wafua vyuma na shaba wa kuitengenezatengeneza Nyumba ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme na Yoyada walitoa feza zile na kuwapa wale waliosimamia kazi ya kujenga upya nyumba ya Yawe. Nao wakalipa wajengaji, waseremala kwa kutengeneza nyumba ya Yawe. Wakalipa vilevile wafuaji wa chuma na shaba kwa kujenga upya nyumba ya Yawe.