2 Chronicles 24:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipomaliza kuitengeneza nyumba ya Mwenyezi-Mungu, walimletea mfalme na Yehoyada dhahabu na fedha iliyobaki; halafu vyombo kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vilitengenezwa kwa fedha hizo, vyombo hivyo vilikuwa vya kutumika katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, matoleo ya sadaka za kuteketeza na mabakuli ya kufukizia ubani, pia vyombo vya dhahabu na vya fedha. Watu waliendelea kutoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakati wote wa utawala wa Yehoyada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada akiwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya Bwana, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Bwana, daima, siku zote za Yehoyada.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipomaliza kuitengeneza nyumba ya Mwenyezi-Mungu, walimletea mfalme na Yehoyada dhahabu na fedha iliyobaki; halafu vyombo kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vilitengenezwa kwa fedha hizo, vyombo hivyo vilikuwa vya kutumika katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, matoleo ya sadaka za kuteketeza na mabakuli ya kufukizia ubani, pia vyombo vya dhahabu na vya fedha. Watu waliendelea kutoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakati wote wa utawala wa Yehoyada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la BWANA: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la bwana: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipomaliza kuitengeneza nyumba ya Mwenyezi-Mungu, walimletea mfalme na Yehoyada dhahabu na fedha iliyobaki; halafu vyombo kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu vilitengenezwa kwa fedha hizo, vyombo hivyo vilikuwa vya kutumika katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, matoleo ya sadaka za kuteketeza na mabakuli ya kufukizia ubani, pia vyombo vya dhahabu na vya fedha. Watu waliendelea kutoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakati wote wa utawala wa Yehoyada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha wakazipeleka fedha zilizobaki kwa mfalme na kwa Yoyada, wakazitumia kutengeneza vyombo vya Nyumba ya Bwana, ni vyombo vya kutumia, walipotoa ng'ombe za tambiko, na vyano na vyombo vingine vya dhahabu na vya fedha, kisha wakamtolea Bwana katika Nyumba ya Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima pasipo kukoma siku zote za Yoyada.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, daima, siku zote za Yehoyada.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipomaliza kutengeneza nyumba ya Yawe, wakamuletea mufalme na Yoyada zahabu na feza iliyobaki; halafu vyombo kwa ajili ya nyumba ya Yawe vilitengenezwa kwa feza hizo, vyombo hivyo vilikuwa vya kutumika katika kazi ya nyumba ya Yawe, matoleo ya sadaka za kuteketeza kwa moto na mabakuli ya kufukizia ubani, vilevile vyombo vya zahabu na vya feza. Watu waliendelea kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto katika nyumba ya Yawe wakati wote wa Yoyada.